Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba leo August 2, 2017 ameagiza magari na boti ambazo zimetumika kusafirishia wahamiaji haramu zichukuliwe na watu wanaowalipia faini nao wajumuishwe katika kosa hilo.
Akiwa katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Pwani kukagua Kiwanda cha Vitambulisho vya Taifa, NIDA na Ofisi ya Uhamiaji Pwani, Waziri Mwigulu amesema mtu ambaye atawalipia faini wahamiaji haramu ili waachiwe naye ajumuishwe na vifaa ambavyo vimetumika kuwasafirishia vichukuliwe na kupelekwa Magereza na Idara nyingine zenye uhitaji wa vifaa.
ULIPITWA na hii kauli ya Waziri Mwigulu Nchemba kusema “Hatuombi watu kuacha uhalifu, tunawaambia tutapambana nao”…tazama kwenye video hii!!!
Kitu Waziri Mwigulu amewaambia Watanzania kuhusu JPM, Makinikia…tazama kwenye video hii!!