Kikao cha halmashauri kuu ya Taifa ‘NEC’ ya chama cha mapinduzi ‘CCM’ kimekutana leo December 13 2016 ikulu jijini Dar es salaam ikiwa ni kikao cha kwanza kuongozwa na Rais Magufuli tangu achaguliwe kukiongoza chama hicho tawala July mwaka huu. Hizi ni baadhi tu ya kauli alizozitoa mwenyekiti wa chama hicho Rais Magufuli
'Sioni aibu ya kuwakaribisha wanaCCM hapa Ikulu maana bila ninyi nisingefika hapa, hapa ni mahali pa watanzania wote'-JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Vyama vingine wakitaka kufanya vikao hapa Ikulu waombe ila tutataka kujua ajenda zao'-JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Hii haitakuwa mara ya mwisho tutakapoamua hakuna mtu atakayenipangia nifanyie mkutano wapi'-JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Hatutaki kuwa na chama legelege cha watu walalamikaji, sisi ndio tumepewa ridhaa na wananchi kuongoza'-JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Nitapenda chama changu CCM kizingatie kanuni za uchaguzi ikwemo kanuni ya kiongozi kuwa na nafasi moja tu ya uongozi-JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Nitapenda kuwa na jumuiya za chama zinazozingatia matakwa ya chama'- JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Napenda tuwe na chama kinachoongozwa na wanachama na sio chama kuongozwa na mtu chama ni mali ya wanachama'- JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Tunataka kununua meli mbili, moja ziwa Tanganyika na nyingine ziwa Victoria' -JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Tunataka chama chetu kijitegemee kiuchumi, ni aibu kutegemea fedha za ruzuku na watu binafsi ili kujiendesha' -JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Rasimali nyingi hatunufaiki nazo kutokana na mikataba isiyo na tija, usimamizi mbovu na ubadhirifu'-JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Wapo wananchama wachache ambao ukisaliti chama chetu hasa kipindi cha uchaguzi na wengine kuendeleza makundi'-JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Napongeza kamati za siasa za wilaya, mikoa ambazo zimechukua hatua dhidi ya waliotusaliti kwenye uchaguzi mwaka jana-JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Katika awamu hii hatutamsamehe mtu yeyote wa kutafuta uongozi kwa njia ya rushwa' JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Nina uhakika zaidi ya viwanja sita katika nchi hii tutaviwekea lami, tumeanza na Dodoma'-JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Bei ya korosho imepanda kutoka 1000 hadi 4000 kwa kg 1 na walivyo wale watani zangu wameamua kuwanywesha mbuzi bia-JPM #HalmashauriKUUCCM

'Nimeshapata mialiko karibu ya 50 lakini nimeamua kusafisha nyumba yangu kwanza kabla ya kwenda kusafisha kwa jirani'-JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Tunaposema yaliyopita si ndwele tugange yajayo sio kwamba tumeyasahau yaliyopita, niwaombe tuendelee kukijenga chama-JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Zile nafasi za mwenyekiti kuchagua wajumbe wa NEC zimepungua, badala ya 10 nitachagua 7, lengo kutengeneza mwelekeo wa chama kipya'- JPM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
'Nawaomba mtembee kifua mbele ninyi ndio watawala, hakuna chama kingine tawala'-JPM #HalmashauriKUUCCM
— millardayo (@millardayo) December 13, 2016
AyoTVMAGAZETI: Miili kwenye viroba yamuibua Mwigulu, Mambo 6 pasua kichwa kikosi timu mpya CCM, Bonyeza play hapa chini