Club ya CD De Agosto ya Angola imetumia ukurasa wake wa instagram kuandika malalamiko yao kwa kudai kuwa wenyeji Namungo FC wanadhoofisha kikosi chao baada ya kupewa majibu kuwa wachezaji watano wa De Agosto hawawezi kucheza leo wana Corona.
Wachezaji wa De Agosto wanaoripotiwa kuwa na Corona ni golikipa Nebi, Bobo, Boni, Mario, Mabululu pamoja na mratibu wa timu Untonesa Sampaio.
Mchezo huo utakaochezwa leo Chamazi ambapo De Agosto anahesabika kama mwenyeji baada ya awali kushindwa kuchezwa nchini Angola kutokana na kudaiwa wachezaji na CEO wa Namungo FC kuwa na Corona.