Mix

Viongozi wa CHADEMA waliohukumiwa miezi 8 jela kwa kufanya mikutano bila kibali

on

Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimethibitisha kwamba viongozi wake wawili kati ya 18 waliokamatwa na Polisi mwaka 2016 na baadae 6 kati yao kupelekwa Mahakamani, wamehukumiwa kwenda jela.

Tumaini Makene ambaye ni mkuu wa idara ya habari na mawasiliano CHADEMA amesema viongozi hao wawili wamehukumiwa kwenda jela miezi nane bila faini kwa kosa la kufanya mikutano bila kibali na waliohukumiwa ni Mwenyekiti CHADEMA Lindi, Suleiman Luwongo na Katibu wa tawi la Nyamagara.


ULIPITWA? Tazama hapa chini Freeman Mbowe akizungumzia kukamatwa kwa Edward Lowassa Geita na kuhojiwa.

Soma na hizi

Tupia Comments