Wanasayansi Uingereza wameonya tabia ya wanafunzi kunywa pombe hasa kwa kupindukia na kuwa suala hilo lina madhara makubwa kwenye ufanyaji kazi wa ubongo.
Imeelezwa kuwa kwa wanaume kunywa bia tano au zaidi au bia nne au zaidi kwa wanawake ndani ya masaa mawili huzorotesha uwezo wa akili kufanya kazi hususani katika kuprocess taaarifa mbalimbali.
Pia wanasayansi hawa wameeleza kuwa unywaji wa pombe uliopindukia kwa wanafunzi husababisha kutofanya vizuri kitaaluma pamoja na kuchochea wanafunzi wengi kujihusisha na tabia hatarishi kama ngono zembe na nyinginezo.
Ulipitwa na hii? Upelelezi wa kesi ya Halima Mdee wa kumtolea lugha ya matusi Magufuli umekamilika
Hii je? Ofisi nyingine za mawakili zavamiwa Dar es salaam