Ni July 26, 2021 ambapo Mbunge wa Nzega Vijini, Hamisi Kigwangalla anamiliki vichwa vya habari baada ya kusema Chanjo ya kujikinga na Ugonjwa wa Corona (Covid-19) ni salama.
Mbunge huyo kupitia ukurasa wake wa twitter aliyaandika haya..”Usijiulize ukapate chanjo gani. Siyo swali la muhimu sana Kwa sasa. Chanjo zote ni salama na zinafanya kazi. Chanjo zimefanyiwa utafiti na hazina madhara yoyote yale ya kutisha kwa binadamu. Chanjo yoyote itakayokuja mbele yako, ipokee. Itumie!”-Hamis Kigwangalla
“Nimelala salama na nimeamka salama. Alhamdulillah. Kila kitu kiko sawa, hakuna kilichopungua wala kuongezeka mwilini zaidi ya ‘amani ya moyo’. Niko vizuri, ikiwa ni masaa zaidi ya 40 toka nipate chanjo ya Corona. Chanjo ni salama kabisa! Jiandae kupata chanjo yako.“-Hamis Kigwangalla
CORONA TANZANIA: VIFO 29, WAGONJWA WAPYA 176 NDANI YA SIKU MOJA
MWIJAKU ANAITAKA KAZI YA MANARA SIMBA ” SIFA NINAZO”