Uongozi wa klabu ya Chelsea December 16 iliripotiwa kuweka kikao cha dharura kujadili mwenendo wa timu yao kwa sasa, Chelsea baada ya kukaa kikao hicho cha bodi, December 17 walitangaza rasmi kumfuta kazi Jose Mourinho na nafasi yake kubaki wazi.
Stori mpya ni kuwa uongozi wa klabu ya Chelsea December 19 umetangaza rasmi kumteua kwa mara ya pili Guus Hiddink kuwa kocha wa muda wa kukinoa kikosi. Chelsea imemfukuza Mourinho baada ya kuiongoza kucheza mechi 16 za Ligi Kuu Uingereza msimu huu, kufungwa tisa, sare mitatu na kushinda minne.
Hii sio mara ya kwanza kwa Chelsea kumteua Guus Hiddink kuwa kocha wa muda wa klabu hiyo, lakini sio mara kwanza kwa Chelsea kumfukuza Jose Mourinho. Kwa mara ya kwanza Chelsea ilimteua Guus Hiddink kuwa kocha wa muda mwaka 2009, lakini kwa upande wa Mourinho kwa mara ya kwanza alifutwa kazi akiwa na Chelsea mwaka 2007.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.