Ligi Kuu Uingereza iliendelea usiku wa March 1 kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja tofauti tofauti, miongoni mwa mchezo uliochezwa usiku wa March 1 ni mchezo kati ya Norwich City dhidi ya Chelsea katika dimba la Carrow Road.
Chelsea walikuwa ugenini na kuendeleza harakati zao za kupambana na kuhakikisha wanashika nafasi za juu, licha ya kuwa matumaini yao ya kutetea taji lao la Ligi Kuu Uingereza yameshapotea, kwani wana tofauti ya point 18 dhidi ya Leicester City anayeongoza Ligi.
Usiku wa March 1 dimba la Carrow Road Chelsea walifanikiwa kuondoka na point tatu muhimu, baada ya goli la dakika ya kwanza la Robert Kenedy na goli la dakika ya 45 la Diego Costa kudhihirisha ushindi, licha ya jitihada za Norwich City kutaka kusawazisha kwa Nathan Redmond kuifungia goli la kwanza dakika ya 68.
Chelsea ambao walifanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-1, wapo nafasi ya 8 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza kwa kuwa na jumla ya point 39 katika michezo ya 28 waliocheza. Chelsea watashuka dimbani March 5 kucheza dhidi ya Stoke City katika mchezo wao wa 29 wa Ligi Kuu Uingereza.
Video ya magoli ya Chelsea Vs Norwich City
https://youtu.be/3989aPzfDN0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE