Ligi Kuu Uingereza imeendelea tena usiku wa December 14 kwa mchezo mmoja kupigwa katika dimba la King Power, timu zote za Ligi Kuu Uingereza zilikuwa zimecheza mechi 16 kila moja kasoro timi za Leicester City na Chelsea ambazo zenyewe ndio zimepambana usiku wa December 14.
Huu ulikuwa ni mchezo wenye mvuto kwani Leicester City ambao walikuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, walikuwa wanahitataji ushindi ili kuendelea kukaa kileleni na kuishusha Arsenal ambayo ilikuwa imekaa hapo kutokana na kuizidi michezo Leicester City.
Licha ya kuwa Leicester City ni klabu yenye jina ambalo sio maarufu kama Chelsea, imeendeleza rekodi yake ya kucheza michezo 16, kushinda michezo 10, sare michezo mtano na kupoteza mmoja, kipigo cha Leicester City cha goli 2-1 kwa Chelsea kinafanya Chelsea kutimiza idadi ya mechi tisa ilizofungwa msimu huu.
Chelsea walianza kufungwa na mshambuliaji aliyevunja rekodi ya mkongwe wa Man United Ruud van Nistelrooy iliyodumu kwa miaka 12 Jamie Vardy dakika ya 34 na kipindic cha pili dakika ya 48 mmoja kati ya wachezaji walioifunga Taifa Stars dhidi ya Algeria Riyad Mahrez akapachika goli la pili ila dakika ya 77 Loic Remy akafunga goli la kwanza kwa Chelsea, goli ambalo liliwafanya Chelsea kupata nguvu licha ya kuwa hakufanikiwa kusawazisha.
Video ya magoli ya Leicester City Vs Chelsea
https://youtu.be/xNa-q6ECu7Y
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.