Michezo

Baada ya kumkosa John Stones, Chelsea yamsajili beki huyu wa Senegal kutokea Ufaransa

on

Klabu ya Chelsea ya Uingereza ambayo kwa siku za hivi karibuni imekuwa ikituma ofa zaidi ya tatu za kuomba kumsajili beki wa klabu ya Everton ya Uingereza John Stones bila mafanikio, Septemba 1 imekamilisha mpango wa kumsajili beki wa kimataifa wa Senegal aliyekuwa anakipiga katika klabu ya FC Nantes ya Ufaransa Papy Djilobodji.

che

Kwa mujibu wa mtandao wa telegraph Papy Djilobodji mwenye umri wa miaka 26 amesaini mkataba wa miaka minne kuitumikia Chelsea kwa ada ya uhamisho ya pound milioni 2.7. Papy Djilobodji alijiunga na FC Nantes mwaka 2010 akitokea klabu ya US Sénart-Moissy, hata hivyo huyu ndio anatajwa kuwa mbadala wa John Stones.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikiaza siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments