Polisi wamesema wamemkamata mwanamume mwenye umri wa miaka 25 kwa jina la Wu katika mji wa Lianjiang kwa kuhusika na shambulio hilo.
Wahasiriwa wengine ni mwalimu na wazazi wawili, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa afisa wa eneo hilo. Mtu mmoja pia amejeruhiwa.Polisi wametaja tukio hilo kama “shambulio la kukusudia.”
Shambulio hilo lilitokea mapema leo Jumatatu wakati wazazi walipokuwa wakiwapeleka watoto wao kwa ajili ya masomo.
Silaha za moto zimepigwa marufuku nchini China lakini nchi hiyo imeshuhudia mashambulio mengi ya visu katika miaka ya hivi karibuni, ingawa pia kulikuwa na tukio moja ambapo mshambuliaji alitumia dawa ya kemikali kujeruhi watoto 50 waliokuwa darasani.
Mwezi Agosti mwaka jana, mshambuliaji mwenye kisu alivamia shule ya chekechea katika mkoa wa Jiangxi kusini-mashariki wa China na kuua watu watatu na kujeruhi wengine sita.
Mnamo Aprili 2021, watoto wawili walikufa huku wengine 16 wakijeruhiwa wakati wa shambulio la watu wengi katika mji wa Beiliu, katika mkoa unaojitawala wa Guangxi Zhuang.
Oktoba 2018, watoto 14 walijeruhiwa katika shambulio la kisu katika shule ya chekechea huko Chongqing, kusini-magharibi mwa China.