Miongoni mwa vitu vikubwa vilivyowahi kusikika kwenye headlines kutokea upande wa China vikihusisha raia wa Afrika Mashariki ni pamoja na Watanzania kusachiwa kwa zaidi ya dakika 60 kwenye vyumba maalum kwenye viwanja vya ndege sababu ya rekodi za kuingiza dawa za kulevya kwenye taifa hilo.
Sasa kingine ambacho Maafisa wa uhamiaji kwenye mji wa Xiamen huko China wamekidaka ni cha jamaa mmoja raia wa China kukamatwa na meno ya Tembo yenye thamani ya zaidi ya bilioni mbili za Kitanzania ambapo alipohojiwa amesema ametoka nayo nchini Uganda na kilo moja aliinunua kwa zaidi ya shilingi laki sita za Kitanzania.
Serikali ya China ambayo inaungana na mataifa mengine duniani kwenye kupinga uwindaji haramu kampeni ambayo ina mabalozi akiwemo mwimbaji wa Bongofleva Alikiba, imesema kwenye kamatakamata ya mwaka 2015 hiki ndio kiwango kikubwa cha meno ya Tembo kilichokamatwa nchini humo.
Meno haya ya Tembo yalikua yamewekwa kwenye mabegi matatu ndani ya kontena lililosafirishwa kutokea Uganda na mtuhumiwa ni Bwana Huang ambaye anaweza kufungwa kuanzia miezi sita mpaka maisha Jela kutokana na kosa kama hili.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE