Mix

Wachina na njia mpya za kulipa bili za vyakula…

on

Najua kuna wale watu wangu wanaopenda kutoka kila weekend kula good time na watu wao huku wakipiga stori mbili tatu.. lakini ikifika wakati wa kulipa watu wanakimbia bili na usipokaa vizuri utajikuta bili ya watu wote unalipa wewe.

Wachina wameona hili ni tatizo kwa vijana wengi sana ambao labda kwa namna moja ama nyingine wanalazimika kuonyesha kiasi cha pesa wanachochangia pale bili inapokuja mezani na pengine kuona aibu kuhofia labda wakichangia pesa ndogo watachekwa, hivyo wameamua kuleta kitu kinachoitwa ‘WeChat Communication Tool’.

weChat

Hii ikoje? WeChat Communication Tool ni application ya kuchat kama vile ilivyo Whatsapp lakini tofauti ni kwamba kwa kutumia application hii unaweza kulipia bili ya chakula kwa kupiga picha kile unachotaka kuchangia kulipa na kuituma kwenye ‘WeChat Wallet’ na kumaliza kila kitu huko bila kutoa pesa yako mfukoni!

weChat

WeChat Payment Wallet.

Zaidi ya watu million 600 China wanatumia hii application sio tu kwa kulipia chakula bali hata kwa huduma nyingine ndogondogo kupitia simu zao za mikononi, lakini huduma ya ulipaji wa bili za vyakula kwa kuchangia kupitia WeChat Wallet ilianza rasmi mwaka jana na toka kipindi hicho idadi ya watumiaji wamekuwa wakiongezeka kila siku.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments