Baada ya zile taarifa kuenea Duniani kote kupitia mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari kwamba huu sasa ndiyo mwisho wa Chris Brown na aliyekuwa mpenzi wake Karrueche Tran wameachana, ikufikie taarifa hii kwamba siku ya leo Desemba 07 walitumia kurasa zao zilizopo katika mitandao ya kijamii hasahasa Instagram kila mmoja kuzungumza alichonacho moyoni kuhusu mwenzake.
Chris Brown alipost ujumbe ulioonyesha namna ambavyo hakupendezwa na kitendo cha Karrueche kumtembelea mara moja tuu alipokuwa amefungwa gerezani kutokana na kesi yake na pia zile tetesi za kwamba Karrueche ana mahusiano na Drake, lakini Karrueche hakukaa kimya, alijibu kwamba hakupendelea kuendelea na uhusiano ambao haukuwahi kumpa furaha.
Kwenye mtandao wa Youtube kuna video inayomwonyesha Chris akiuliza “How many single ladies we got in here tonight?… Well, I’m single too…”
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook