Mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa aliyekuwa anaichezea klabu ya Liverpool ya Uingereza Djibril Cisse October 20 ameingia kwenye headlines baada ya kufanya maamuzi ambayo wanasoka wengi huchukua muda kuyafanya. Djibril Cisse ambaye amewahi kutamba katika vilabu kadhaa vikubwa Uingereza ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 34.
Djibril Cisse amewahi kushinda mataji 41 katika soka akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa na amewahi kucheza soka katika vilabu 12 katika kipindi cha muongo mmoja na nusu. Uamuzi wa Djibril Cisse kustaafu soka haukuwa rahisi kama ambavyo wengi wangeweza kutarajia, kwani staa huyo alitangaza uamuzi huo huku machozi yakimtoka katika mahojiano ya TV.
Ulimwengu wa soka bado utaendelea kumkumbuka Djibril Cisse kwa kuisaidia Liverpool kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini amewahi kutwaa tuzo ya kiatu cha dhahabu mara mbili akiwa Ufaransa na Ugiriki. Staa huyo wa soka amewahi kucheza katika vilabu 12 vya soka vikiwemo Liverpool, Sunderland na QPR. Cisse ambaye ametangaza maamuzi hayo nafsi yake ikiwa bado inatamani kuendelea kucheza soka amekubali yaishe kutokana na umri kumtupa mkono.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.