Naibu Waziri wa Elimu William Ole Nasha jana March 1, 2018 alikuwa mkoani Mara katika ziara ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya shule inayoojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia programu ya lipa kulingana na matokeo (EP4R).
Katika ziara hiyo Ole Nasha ametoa onyo kwa walimu wote nchi wanaojihusisha kimapenzi na wanafunzi na kuwaambia waache mara moja tabia ya kuwarubuni wanafunzi badala yake warudishe nidhamu ya wanafunzi na kuinua kiwango cha elimu na ufaulu katika shule wanazofundisha.
Ole Nasha amesema amepokea taarifa juu ya baadhi ya walimu kujihusisha kimapenzi na wanafunzi wao jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi pamoja na maadili ya utumishi wa umma.
Ameeleza kuwa serikali haitamvumilia mwalimu yeyote mwenye tabia kama hizo na kuongeza kuwa mwalimu atakayebainika kushiriki vitendo hivyo atashtakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi pamoja na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kulingana na taratibu za utumishi wa umma.
Pia amewataka wazazi na walezi kuhakikisha hawajihusishi kwa namna yoyote kupokea fedha ili
kuwaficha wahalifu wanaokatiza masomo ya watoto wao kwa kuwapa ujauzito badala yake waache
sheria ichukue mkondo wake ili kusaidia kukomesha vitendo hivi viovu katika jamii.
Nae Mkuu wa wilaya ya ya Musoma Dk Vicent Naano amesema wilaya yake inakabiliwa na tatizo la mimba za utotoni ambapo kwa mwaka wastani wa wanafunzi mia moja wanapata ujauzito na kukatiza masomo.
“Watu hawana elimu kuhusu KUBEMENDA watoto” –Waziri Jafo