Michezo

Mashabiki wa England wafanya jambo hili kumzuia Cleverley kuichezea timu hiyo

on

article-2569367-1984A99F00000578-286_634x396Jumla saini 6,000 za mashabiki wa soka nchini England zimekusanywa katika ombi maalum la kumtaka na Chama cha soka cha nch hiyo FA pamoja na kocha Roy Hodgson kutomuita kiungo wa Manchester United Tom Cleverley katika kikosi cha nchi hiyo kitakachoenda kushiriki michuano ya kombe la dunia nchini Brazil mwaka huu.

Ombi hilo la mashabiki lilikusanya saini zisizopungua 4,000 ndani ya masaa 24.

Ombi hilo lilikuwa na ujumbe ufuatao

article-2570211-1BE9F76200000578-467_634x497

Kama ilivyo kwa wachezaji wenzie wengi, Cleverley ameshindwa kurudia kiwango chake kizuri alichokuwa nacho miaka miwili iliyopita, kilichomfanya Sir Alex Ferguson kumuita ‘special player’

Cleverley amefunga goli moja tu katika michezo 32 aliyoichezea klabu yake na amekuwa akisemwa mpaka na mashabiki wa timu yake, hasa kwenye mtandao wa Twitter.

Pamoja na kusemwa sana, kiungo huyo mwenye miaka 24 amechaguliwa na kocha Hodgson alhamisi iliyopita kuunda kikosi cha Denmark wiki hii, na inaonekana ana nafasi ya kwenda Brazil.

Tupia Comments