Premier Bet
TMDA Ad

Mix

Mauaji yametokea ndani ya nyumba ya Sinema Marekani, kilichofuatia? Stori na video hapa..

on

cinema5

Saa chache ziliyopita kumetokea tukio la mauaji Marekani ambako mwanaume mmoja aliamua kupiga risasi ovyo akiwa kwenye nyumba ya Sinema iliyopo Lafayette Louisiana na kusababisha vifo vya watu 2 na majeruhi ya watu 9 kabla ya kujiua yeye mwenyewe.

Tukio hilo limewashtua na kuwatisha watu wengi ambao wanadai hawaoni kama kulikuwa na sababu ya mtu huyo kufanya hicho alichokifanya.

cinema

Mwanaume huyo ambaye jina lake halijafahamika alikuwa na umri wa miaka 58 na kutokana na ushuhuda wa wafanyakazi wa eneo hilo la sinema alikuwa ni mhudhuriaji mzuri wa sehemu hiyo mara kwa mara.

Polisi wanaendelea na upelelezi juu ya hilo tukio ikiwemo kumtambua huyo jamaa pamoja na ndugu ama familia yake.

cinema4

Polisi wanasema zaidi ya watu 100 walikuwemo ndani ya sehemu hiyo ya sinema kwa ajili ya kuangalia movie mpya ya Comedy “Trainwreck” kabla ya tukio la mashambulizi ya risasi kuanza.

Tukio hilo lilitokea kwenye mida ya saa 8:30 usiku jijini Lafayette Louisiana Marekani.

Stori iko pia kwenye hizi video hapa.

Soma na hizi

Tupia Comments