Stori Kubwa

Hatimaye CNN imeiomba Kenya msamaha (+Video)

on

FabozSiku chache kabla Rais Obama hajatua Kenya kulikuwa na Ripoti ambayo Kituo cha CNN waliirusha, kwenye Ripoti hiyo waliielezea Kenya kama moja ya nchi ambazo ziko kwenye ‘Ukanda wa Ugaidi’.

Stori ikateka mijadala kwenye Mitandao ya Kijamii, watu wa Kenya hawakupenda CNN walivyoitaja vibaya nchi yao, kingine kiliibuka kama wiki mbili zilizopita ambapo Bodi ya Utalii Kenya ilisimamisha kurusha Matangazo yao ya Utalii yaliyokuwa yakirushwa kwenye Kituo cha CNN!!

wpid-img_20150813_190431-710x434

Tony Maddox na Rais Uhuru Kenyatta

Alhamisi August 13 2015 moja ya Maboss wa CNN, Tony Maddox amesafiri toka Atlanta Marekani Makao Makuu ya CNN na kuingia Ikulu ya Kenya, Nairobi na kufanya kitendo cha kiungwana kuomba radhi kutokana na CNN kuitangaza vibaya Kenya >>> “Tunajua hiyo Ripoti iliwakasirisha wengi ndio maana baada ya kugundua tuliiondoa hewani haraka… Haikuwa na maana ya kuipa sifa mbaya Kenya, tunakili kosa hilo… kuna maeneo ambayo yana machafuko na Ugaidi lakini Kenya huwezi kuiweka kwenye kundi la Nchi hizo…”—Tony Maddox.

Baada ya kumsikiliza Tony, Rais Kenyatta nae alitolea majibu haya >>> “CNN kuielezea Kenya kama sehemu ya Ukanda wa Ugaidi inavunja moyo na kushusha ari ya Vikosi vya Kenya vilivyojitoa kupambana na Ugaidi, ndio maana sauti ya Wakenya ilibebwa na walioingia Twitter na kukosoa… walikasirishwa sana, Kenya sio nchi iliyo kwenye Vita, hakukuwa na maana kuijumuisha Kenya kwenye upande huo” >>> — Rais Uhuru Kenyatta.

Story hiyo nimeipata pia kwenye Channel ya Youtube ya Kituo cha TV cha NTV Kenya, unaweza kuplay uisikilize pia.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments