Bado mambo ni magumu India baada ya Waziri Mkuu wa Nchi hiyo Narendra Modi kutangaza lock down ya siku 21 kuanzia March 24,2020 kujikinga na corona, Irene Julius ni Mtanzania anaesoma India na anasema hakuna anayeruhusiwa kutoka nje ya nyumba yake, Askari wakikuona nje bila sababu ya msingi unatandikwa bakora.
“India kuna complete lock down, Watu hawaendi kazini, wanafunzi hawaendi shule, maduka yamefungwa, natamani ningerudi nyumbani Tanzania ila ndege hamna, ukitoka nje Askari wanapiga Watu, tupo ndani kama tupo Gerezani”– Irene Julius