Kwa mara ya kwanza katika historia, bei ya mafuta ghafi imeshuka chini ya Dola 0. Bei ya nishati hiyo imekuwa ikiporomoka tangu mapema mwaka huu na kutokana na mlipuko wa COVID 19, uhitaji umeshuka kwa kiasi kikubwa.
Virusi ya Corona vimepunguza matumizi ya mafuta kusababisha bei kushuka kwa kasi huku wazalishaji wakilazimika kuhifadhi mafuta yasiyotumika. Hali imekuwa mbaya zaidi kwa mataifa makubwa ambapo Soko la Hisa limeathirika.
Hapo jana, bei ilishuka kutoka Dola 12 hadi Dola 4 kisha ikashuka tena mpaka Dola 2, na watu wamekuwa wakijadili mitandaoni wakisema kikombe cha kahawa kina gharama zaidi kuliko pipa la mafuta ghafi.
Siku chache zilizopita Donald Trump alidai kuwa ameokoa sekta ya nishati na amefanya makubaliano makubwa zaidi ya mafuta.