Wilaya ya Kisarawe chini ya DC wake Jokate Mwegelo imefanikiwa kuzalisha mavazi ya kujikinga na corona (PPE) ambayo yanatengenezwa katika Hospitali ya Wilaya hiyo, tayari mavazi zaidi ya 200 yametengenezwa kwa ajili ya wahudumu wa afya wa Wilaya hiyo na sasa Kisarawe imeanza uzalishaji wa mavazi mengine ambayo yatasambazwa kila kona ya Tanzania.
“Kwa siku tunatengeneza mavazi (PPE) zaidi ya 100, lengo letu ni kuisaidia Tanzania nzima, tunatengeneza barakoa na sanitizer pia na kazi zote zinafanywa na Vijana wa Kitanzania, ukinunua PPE nje bei inafika hadi laki tatu, tukaona tutengeneze ili kuisaidia Nchi kuokoa mapato, vazi moja halizidi Elfu 50”– MGANGA MKUU WA HALMASHAURI