Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema hakuna maambukizi mapya ya ndani kwa siku nyingi Uganda na kusema huenda hiyo ina ashiria hakuna maambukizi tena ya corona au Watu wana virusi ila hawaugui , Museveni amesema kwa mujibu wa Wataalamu wake kama Watu wana virusi na hawaugui ni jambo zuri kwakuwa wanapata kinga mwili na hata virusi vikiondoka vikarudi tena watapambana navyo.
“Bado tuna visa 79, wagonjwa wanapona kwa kasi hadi sasa wamepona 52 na hatuna kifo, visa vya ndani tumedhibiti kabisa, tuko vizuri, shida pekee kwa sasa ni visa vya nje vinavyoletwa na Madereva wa Malori, naambiwa Waganda wana hasira nao kweli, tusiwachukie jirani zetu”-MUSEVENI
KIM JONG UN AMEJIFICHA KUKWEPA CORONA, TRUMP ASEMA ANAJUA KILA KITU “NIMEZUIA VITA YA USA NA KOREA”