Licha ya picha zake za awali kumuonesha Cristiano Ronaldo akiwa katika ndege kuelekea Ureno kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Ureno, Ronaldo hakuishia kuungana na timu pekee kwani alitumia muda wake akiwa Ureno kuzindua brand mpya ya viatu vyake.
Ronaldo anaonekana kujikita zaidi katika biashara kama za mavazi perfume na kadhalika kwa kutumia umaarufu wake, kwani inaweza ikawa rahisi zaidi kufanikiwa, awali Ronaldo alizindua nguo za ndani, mashati, perfume na sasa ni wakati wa kuzindua viatu vyake, huenda ukawa unajiuliza model gani anayemtumia kuuza bidhaa zake.
Staa huyo wa Real Madrid ya Hispania amesimama mwenyewe kama model wa bidhaa zake, kuanzia nguo za ndani, perfume, shati na hata sasa viatu. Cristiano Ronaldo anaingia katika list ya watu maarufu waliowahi kuanzisha na kuuza bidhaa zao kwa kutumia majina yao. Brand mama ya Ronaldo ni CR7
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE