Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Kuna hii ya wanafunzi chuo Kikuu kuanza kusoma kuhusu staa Cristiano Ronaldo !!

on

cristiano-ronaldo-hairstyle-4-1024x576

Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo ameendelea kuwa maarufu duniani baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza umri wa miaka 30.

Mchezaji huyo wa Real Madrid hivi karibuni huenda akajikuta akitumiwa katika elimu ya chuo kikuu baada ya chuo cha British Columbia Okanagan kuanzisha kozi ambayo itakuwa na masomo yanayomhusu nyota huyu.

Chuo hiki kitaanzisha kozi ya shahada ya juu ya Sociology ambayo itakuwa inasomwa na wanafunzi kwa muda wa miaka minne huku wanafunzi hao wakijikita kwenye umaarufu wa nyota huyu na jinsi ambavyo anaathiri watu mbalimbali duniani na utamaduni kwa jumla.

Chuo cha Biritish Columbia Okanagan kilichoko nchini Canada kinataka kuanzisha kozi ya Cristiano Ronaldo .

Chuo cha British Columbia Okanagan kilichoko nchini Canada kinataka kuanzisha kozi ya Cristiano Ronaldo.

Profesa Luis Aguilar ambaye ameanzisha wazo hili amesema kuwa Ronaldo ni mtu mwneye umaarufu wa kipekee na ni muhimu kwa watu kufahamu umaarufu wake unavyowagusa watu tofauti duniani.

Profesa huyo ameongeza kuwa wanafunzi hawatajifunza jinsi ambavyo mchezaji huyo anavyopiga chenga au kufunga mabao akiwa uwanjani bali watajifunza jinsi alivyo na mchango hasi au chanya kwa jamii tofauti ambazo zimejaa watu wanaomfuatilia.

Umaarufu wa Ronaldo ni muhimu kusomwa na wanafunzi wa kozi ya Sosiolojia kwa mujibu wa Professa wa chuio kikuu cha British Columbia .

Umaarufu wa Ronaldo ni muhimu kusomwa na wanafunzi wa kozi ya Sociology kwa mujibu wa Professa wa chuio kikuu cha British Columbia.

Endapo kozi hii itapitishwa na kuanza kutumika rasmi Ronaldo atakuwa mchezaji wa pili wa Real Madrid na Manchester United kutumiwa kama kozi ya chuo kikuu baada ya mchezaji wa zamani wa Madrid na United, David Beckham ambaye ametumika katika masomo kadhaa kwenye chuo cha Strefordshire huko Uingereza.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments