July 04 2016 maeneo ya Maweni-Kintiku Singida mabasi mawili ya kampuni ya City Boys yaligongana na kusababisha vifo vya watu 30 na majeruhi 54.
Tukio hilo limekuwa ni moja ya matukio makubwa yaliyotokea mwaka huu ambalo haliwezi kusahulika, mabasi mengine yaliyopata ajali Super Samy ambalo lilikuwa likitokea Shinyanga kwenda Mwanza baada ya kupinduka na kusababisha vifo vya watu 5 na majeruhi 13 na ajali nyingine ilitokea maeneo ya VETA Dakawa Dodoma july 1 na 2 mwaka huu.
Baada ya ajali kutokea Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA iliyafungiwa baadhi ya makampuni ya mabasi kutoa huduma mpaka watakapotimiza vigezo walivyowawekea, makampuni yaliyofungiwa ni pamoja na kampuni ya mabasi city Boys.
Ripota wa millardayo.com na Ayotv amempata Meneja Mawasiliano wa SUMATRA David Mziray kuhusu kufunguliwa kwa baadhi ya mabasi yaliyokuwa yamefungiwa kutoa huduma…………….
>>>’Mabasi nane na kampuni kadhaa tumeyafungulia baada ya kufungiwa kwa muda kwa kusababisha ajali na madereva wao kukosa sifa lakini sasa yamefunguliwa baada ya kukaguliwa magari yao na madereva wao kutimiza masharti na mabasi ambayo hayajakidhii vigezo yamezuiliwa kutoa huduma’.
ULIKOSA HII MBINU ILIYOGUNDULIWA YA KUWAKAMATA MAJANGILI INAWEZA PIA KUDHIBITI MWENDOKASI WA GARI, UNAWEZA KUANGALIA HAPA CHINI