Baada ya aliyekua mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba kuandika barua ya kutaka kurejea katika wadhifa wake wa uenyekiti.
Jun 17 2016 CUF kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi Taifa Twaha Issa Taslima wamemuomba Prof Lipumba kutowayumbisha kwa maamuzi yake ya kutaka kurejea tena kwenye nafasi hiyo wakati awali aling’atuka, Taslima amesema……
>>>’Chama cha Wananchi CUF kinapenda kuchukua nafasi hii kumuomba Profesa Lipumba kwamba asijaribu kukiyumbisha Chama katika kipindi hiki ambacho nchi ina matatizo makubwa ambapo Watanzania wanahitaji kuwekwa pamoja na kupewa matumaini ya namna gani matatizo yao yanaweza kutatuliwa’
>>>’tutahakikisha Katiba yetu ya Chama na Kanuni zake zinazingatiwa wakati wote na kwamba kila mwanachama atapata haki yake kwa mujibu wa Katiba yetu, hakuna atakayedhulumiwa’
ULIKOSA NUKUU YA MAALIM SEIF ‘LIPUMBA ASAHAU UENYEKITI” ILIVYOTOLEWA UFAFANUZI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE