Kutokea Mbeya weekend hii Naibu Spika Dr Tulia Ackson kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust aliweka mashindano ya Ngoma za Jadi ambapo vikundi mbalimbali kutoka mikoa 15
ya Tanzania vilishiriki huku Washindi walijinyakulia zawadi mbalimbali kama vile pikipiki na pesa taslim ambapo zilitengwa zaidi ya Tsh Milion 51.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura alikuwa mgeni rasmi katika kufunga mashindano hayo.
Sasa good news ni kwamba Taasisi ya Tulia Trust itawasomesha baadhi ya washindi wa ngoma hizo katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo ili kuwaongezea ujuzi zaidi.
Tazama FULL VIDEO hapa chini nimeshakuwekea!!!!
NGOMA ZA JADI! Kitu Wamasai wamefanya mbele ya Dr Tulia Mbeya