fB insta twitter

Waliofukuzwa Chuo Kikuu cha Dodoma waigeukia hii kazi

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini.

Moja ya story kubwa may 30 2016 kwenye gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘Waliofukuzwa UDOM wageukia udadapoa’, Gazeti hilo limeripoti kuwa baadhi ya wanafunzi wa kike waliofukuzwa na uongozi wa chuo kikuu cha Dodoma  ‘UDOM’ wanadaiwa kugeukia biashara ya uchangudoa mjini Dodoma ili kupata fedha za kujikimu na nauli za kuwarudisha kwao .

Gazeti hilo limeripoti kuwa Juzi kupitia kwa Mkuu wa Chuo cha Dodoma, Prof Idrisa Kikula kilitangaza kuwasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7000 wa kozi ya Stashahada ya ualimu ambao hawakuwa na sifa za kusoma masomo hayo. 

Gazeti limedai kuwa juzi jioni eneo maarufu la CDA club lilikuwa na idadi kubwa ya kina dada wanojiuza wengi wao wakiwa ni wanafunzi ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao.

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI MAY 30 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE 

Soma na hizi

Tupia Comments