Hiki ndicho kinachoendelea kuhusiana na kesi inayowakabili Maua Sama na Mtangazaji Soudy Brown ambao walikamatwa na polisi siku kadhaa zilizopita kutokana na kusemekana wamevunja sheria ya Benki Kuu ya Tanzania kwa kutoiheshimu fedha.
Kupitia ukurasa wa twitter wa Wakili Jebra Kambole ameongelea kuhusiana na maombi ya dhamana kuhusu kesi pia inayowakabili Shaffih Dauda na Mx Carter na kusema kuwa mbele ya Hakimu Shaidi dhamana inakuja Jumatatu September 24,2018.
“Kesi ya maombi ya Dhamana Na.13 ya 2018 kati ya Maua Sama, Soudy Brown, Mx Carter, Shaffih Dauda nawengine, Mahakama ya Kisutu mbele ya Hakimu Shaidi inakuja tarehe 24/9/2018”
Nikk Wa Pili kahoji ajali ya MV. Nyerere ‘Ni zoezi la kutafuta miili’