Tunayo story kutokea kwa Wafanyabiashara kutokea nchini DR Congo ambapo wamemuomba Rais John Magufuli kuingilia suala la kuzuiwa kwa mizigo yao katika Bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Leonard Kabeya amesema wanamuomba Rais wa DR Congo, Joseph Kabila azungumze na Rais Magufuli kuhusu suala hilo.
“Tunaomba aingilie kati, kinyume na hapo tutaamia bandari ya Mombasa nchini maana kuna wenzetu washaanza kwenda huko, mizigo yetu inazuiwa bandarini wakati kodi zote tunalipia,“amesema.