Headlines za uamuzi wa Rais wa awamu ya tano Dk John Pombe Magufuli kutangaza kuwa maadhimisho ya siku ya Uhuru kuadhimishwa kitofauti zilichukua sana nafasi katika vyombo vya habari, Siku ya tarehe 9 December ndio siku ambayo Tanzania inakumbuka siku ya Uhuru,
Hivyo badala ya kufanya sherehe na magwaride ya askari, Rais Magufuli alitaka siku hiyo itumike kufanya usafi Tanzania nzima ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu. Agizo hilo la Rais Magufuli lilitekelezwa kwa ufasaha siku ya Jumatano ya December 9 kwa Tanzania nzima kufanya usafi maeneo mbalimbali.
Mtu wangu wa nguvu ikiwa siku mbili zimepita toka Tanzania iadhimishe siku ya Uhuru kwa kufanya usafi, millardayo.com ilitembea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam kukuonesha hali ilivyo katika jiji la Dar Es Salaam, bado baadhi ya maeneo ni masafi kwa kiasi kikubwa ila sehemu chache ndio kuna uchafu kwa kiasi kidogo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.