Kama utakuwa unakumbuka Lina aliwahi kufunguka na kusema kuwa anatamani kuzaa na mwanaume mwenye sifa kama za rapper Darasa, sasa July 6, 2016 Ayo TV ilimtafuta Darasa kuzungumza kuhusu kauli hiyo, Je haikumletea matatizo au aliwahi kuwa na uhusiano na Lina.
Sasa Kupitia Ayo TV Darasa alisema..’Suala la Lina ambacho amekisema ni vitu vya hisia ameonyesha heshima kwanza ningependa kumshukuru na wala sijawahi kuwa nae katika mahusiano labda ya kimapenzi yeye ameweka hisia zake kwamba akiwa karibu na mimi anapata vitu fulani na ndio maana akatolea mfano kwangu lakini sijawahi kuwa na uhusiano na Lina’- Darasa
ULIIKOSA HII YA LINA KUHUSU KUZUNGUMZA TOFAUTI YAKE NA WEMA SEPETU BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA