Wakazi wa Dar es salaam wanaotumia vyombo vya moto kupita Daraja la Mwalimu Nyerere wameanza kulipia fedha kwa viwango vilivyotangazwa na serikali lakini baadhi yao wameomba wapunguziwe wakidai ni kubwa zaidi kwa kuwa mizunguko wanayoifanya kupitia daraja hilo ni mingi.
Gharama ambazo zilitangazwa ilikuwa ni shilingi 1500/= kwa Mikokoteni, Pikipiki, Bajaji na Gari ndogo (Saloon Cars), Magari aina ya Pick-Up yasiyozidi tani mbili yalipangiwa 2000/=, (Minibuses) mabasi madogo yanayobeba abiria wasiozidi 15 yalipangiwa 3000/=, Mabasi yanayobeba abiria kati ya 15 -29 yalipangiwa 5000/=, Tractor 7000/=.
‘Tractor yenye trailer lake yalipangiwa 10,000/=, Magari yenye uzito wa tani 2 mpaka 7 yalipangiwa 7000/=, magari yenye uzito wa tani 7 mpaka 15 yalipangiwa 10,000/=, magari yenye uzito wa tani 15 mpaka 20 yalipangiwa 15,000/=, magari yenye tani 20 mpaka 30 shilingi 20,000/=, Semi Trailer kama magari yanayobeba mafuta 30,000/= na Truck Trailer shilingi 30,000/=
ULIKOSA HII YA TOZO ZA GARI JUU YA DARAJA LA NYERERE? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE