Kituo cha Radio cha Nigeria Info 99.3 kimeripoti kwamba Polisi wa Lagos wamewakamata Wasaidizi wa kazi za nyumbani wa Msanii Davido na wanaendelea kuwahoji kufuatia kifo cha Mtoto wa Mwimbaji huyo aitwae Ifeanyi (3) ambacho kinadaiwa kutokea kwa kuzama kwenye swimming pool.
Hata hivyo pamoja na kwamba kwenye mahojiano hayo Msemaji wa Polisi alithibitisha kutokea kwa kifo hicho lakini alikataa kusema chanzo cha kifo kwa sasa japo mitandao mingi ya Nigeria imeripoti kuwa chanzo ni Mtoto huyo kuzama kwenye bwawa la kuogelea, naendelea kufuatilia zaidi ili kukuletea habari za kuaminika.