Matatizo ya Ardhi ni ishu anbazo kwa mjini yamechukua headlines kila siku, watu wanaoishi ni wengi lakini ardhi ni kama haitoshi kila mmoja kumiliki sehemu yake, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda aliahidi kushughulika nayo toka siuku ya kwanza na leo kuna kipya kutoka kwake.
“Rais J.K kaniteua kuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwangu nilitafsiri kama changamoto kubwa ya kuhakikisha nashughulikia matatizo ya Wilaya hii, nimefuatilia kwa ukaribu sana nimeweza kubaini sababu kadhaa za msingi zinazosimama kama chanzo cha migogoro ya ardhi Kinondoni“>>>
“Pia kama nilivyofanikiwa kubadilisha mfumo wa PF3 ndivyo ninavyofanya kwenye ardhi nimechukua sehemu ya mshahara wangu na kuajiri jumla ya wanasheria watano watakaokuwa wanafanya kazi ya kuwasikiliza na kuwasaidia wananchi kupata haki zao juu ya madai ya ardhi, Wanasheria hawa watalipwa kutoka kwenye mshahara wangu ambapo wananchi wa Kinondoni hawatolipia wanapokuja kupata huduma hii“>>>
“Kila mkazi wa Wilaya yangu anatakiwa kuchukua Copy ya hati au nyaraka yoyote ile inayompa uhalali ya kumiliki ardhi, shamba au kiwanja.. copy hizo zipelekwe kwa mtendaji wa Kata“>>> DC. Paul Makonda.
Hapa utamsikia Mkuu huyo wa Wilaya akiongelea ishu hiyo.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.