Kwa kawaida tumezoea kuona watoto wenye umri wa miaka 15 kuwaona wakiwa elimu ya sekondari hii, imekuwa tofauti kwa mtoto huyu kutoka Thulamahashe Mpumalanga Afrika Kusini kujiunga na chuo cha medicine nchini humo. Mwanafunzi huyo aliyefahamika kwa jina la Decent Junior Mkhombo amejiunga na wanafunzi wenzake kwenye chuo hiko kilichofunguliwa mwaka huu nchini Afrika Kusini kwa lengo la kusomea medicine katika chuo hiko cha University of Limpopo (UL).
Serikali nchini humo imetenga zaidi ya billion 1.3 kwa ajili ya masomo ya wanafunzi wote wanaotarajiwa kujiunga na chuo hiko, ambao baadae watasaidia matatizo ya afya nchini humo. Decent Junior Mkhombo amekuwa mwanafunzi mwenye umri mdogo nchini humo kusomea udaktari lakini mwaka 2014 Dr.Sandile Kubheka alikuwa mwanafunzi wa kwanza kufuzu mafunzo ya udaktari nchini humo akiwa na umri wa miaka 21
“Nina mapenzi ya kujifunza oncology kwa sababu kansa ni ugonjwa mkubwa sana na unatakiwa kupatiwa tiba, kikukweli hatuna maktaba, tuna mahabara kwa jina lakini haina vitendea kazi vya kukidhi, lakini tuna waalimu wazuri kama Mr Richard Walusimbi ambaye amekuwa akitaka tujitume siku zote” >>> Mkhombo
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.