Michezo

Europa League leo tunawajua wanaotinga nusu fainali

on

Chelsea na Arsenal wanaingia katika michezo ya leo wakiwa na matarajio makubwa ya kufuzu kuingia nusu fainali, Arsenal walishinda 2-0 nyumbani kwao dhidi ya Napoli katika mchezo wa kwanza, huku Chelsea wakishinda ugenini dhidi ya Slavia Prague kwa bao 1-0.

Hata hivyo Chelsea walifungwa 2-0 ugenini kwa Liverpool na wako hatarini kumaliza msimu nje ya timu nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, hii inawaongezea sababu zaidi za kupambana ili kushinda taji la Europa.

Mshindi wa Europa hupata tiketi ya moja kwa moja kushiriki Ligi ya mabingwa barani Ulaya na kwa kusema ukweli hapo ndipo Chelsea na Arsenal wanatamani kucheza, Arsenal wanasafiri hadi Italia siku nne tu baada ya kucheza na Watford kwenye ligi na iko wazi kwamba wachezaji wengi hawatacheza kwenye mechi zote mbili kutokana na uchovu na kuepuka majeruhi.

‘Gunners’ walilalamikiwa na mshambukiaji wao wa zamani Paul Mariner, ambaye alisema Arsenal walipoteza nafasi nyingi sana kwenye mchezo wa kwanza. “Cha msingi ni ilikuwa ni kumaliza kabisa mchezo. Walikuwa na nafasi ya kufanya hivyo nyumbani.

Kwenye michezo mingine, Valencia walimaliza nusu ya kazi tayari baada ya kushinda ugenini kwa Villarreal 3-1 na sasa wanaweza kufuzu hata wakipoteza mchezo wa nyumbani kwa magoli machache dhidi ya wenzao wa La Liga, Mchezo mwingine ni Eintracht Frankfurt dhidi ya Benfica Lisbon, huu bado uko wazi kwa timu zote, japokuwa wareno hao walifunga mabao manne, waliruhusu magoli mawili nyumbani pia.

Hii inawapa moyo Frankfurt na matumaini ya kufuzu nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1979/80, walipowafunga Borussia Moenchengladbadch kwa bao la ugenini kwenye robo fainali ya wajerumani (kipindi hicho Europa ilijulikana kama UEFA Cup, game zitaoneshwa ST World Football leo saa 22:00.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments