Dereva wa Lori la mizigo lililokua likitoka Dar es salaam kuelekea nchini Zambia amepata majeraha kidogo baada ya Lori alilokuwa akiliendesha kupinduka maeneo ya Kimara Dar es salaam na kusababisha foleni karibu na eneo la ajali.
Akiongea na Ayo TV Dereva huyo amesema chanzo cha ajali ni kumkwepa bodaboda ambapo Trela ndio likayumba na kusababisha lori hilo kuanguka, Polisi wamewataka Madereva kuangalia njia mbadala wakati jitihada za kuliinua lori zinaendelea.
“Leo nimeanza Safari saa nne wakati natoka nyumbani safi Salama nimekuja mpaka eneo la Kimara nilikuwa natembelea sasa upande wa kushoto ghafla kukawa na bodaboda iliyokuwa imesimama sasa wakati nataka nihamia upande wa Kulia na katika kuhamisha kwangu gari kulia likapanda gema kwahiyo limenichota na kunirudisha kushoto”- Dereva wa Lori
“Nilikuwa naelekea Zambia tangu nianze kazi ya udereva mpaka sasa nina miaka kumi sijawahi kupata Ajali”- Dereva wa Lori
WAFANYAKAZI WATANO WA TRA WAFARIKI KWA AJALI WAKILIFUKUZIA GARI LILILODHANIWA KUWA NA MAGENDO