Mwanamitindo Hamisa Mobetto ambaye pia ni mzazi mwenzake Diamond Platnumz inawezekana akawa mmoja wa watu waliochukua headlines sana kwa mwaka 2017 kutokana na kuzaa na staa wa muziki Diamond platnumz huku awali ujauzito wake akiwa kauweka siri lakini pia kutokana na kutupiana vijembe na Zari kupitia mitandao ya kijamii.
Kupitia Instagram account ya Hamisa Mobetto amepost vitu ambavyo vilimfurahisha kwa mwaka 2017 ikiwemo kupost picha ya mtoto wake wa kiume “Dylan” aliyezaa na Diamond Platnumz na kuandika caption ianyosema “My beautiful 2017 …??@officialprinceabdul ?”
Hamisa Mobetto pia amezidi kudhihirisha kuwa hataki kubeba matatizo ya mwaka 2017 kuingia nayo mwaka mpya wa 2018 na ameandika hili kupitia mtandao wa snapchat “I refuse to step into 2018 with 2017 problems....”
Kutokana na kile alichokiandika Hamisa Mobetto kupitia Snapchat inawezekana kaamanisha kwamba huenda kwa kile ambacho amekifanya kwa Zari kuzaa na Diamond Platnumz ni kosa ambalo hataki lijirudie 2018? Au kutupiana vijembe na zari hataki kuona inajirudia tena 2018?
AUDIO:Kitu H Baba atafanya kama Diamond atamuoa Zari