Mashabiki wa soka ninayo exclusive interview na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambaye anaichezea club ya soka ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta ambaye amefunguka kuhusiana na ishu yake ya kubadilisha namba ya jezi kutoka namba 77 hadi 10.
Mwanzo zilisikika tetesi kuwa Mbwana Samatta baada ya kufika KRC Genk alikuwa akitumia jezi namba 77 lakini baadae akaanza kutumia jezi namba 10 ambayo hata timu ya taifa ndio anaitumia kwa sasa.
Stori zikawa zinasema baada ya viongozi wa Genk kuona uwezo wa Samatta wakamuomba atumie jezi namba 10 ambayo inaaminika mara nyingi inavaliwa na wachezaji ambao wanafanya vizuri au ni mastaa katika club husika, hivyo AyoTV imempata Samatta katika exclusive interview na kuomba ufafanuzi kuhusiana na taarifa hizo.
EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe