Tume ya Vyombo vya Habari Rwanda (RMC) kuanzia wiki ijayo itakaa na kufanyia kazi madai kuhusu maoni yaliyotolewa dhidi ya wanawake na mhubiri kwenye kituo kimoja cha redio nchini humo.
Malalamiko hayo yametolewa na kikundi cha wanawake wanaharakati wa masuala ya wanawake waitwao Pro – Femmes Twese Hamwe. Wanawake hao wamemshtaki mhubiri huyo kwa kusema ‘wanawake ni chanzo cha maovu’.
Mhubiri huyo wa zamani wa Kanisa la Waadventisti Wasabato Nicolas Niyibikora alinukuliwa akisema “Wanawake wako nje ya neema ya Mungu, hakuna kitu kizuri ambacho unaweza kupata kutoka kwa wanawake, kama umesoma biblia, ambaye alileta dhambi ulimwenguni, hakuwa mwanaume.”
“Mkitaka ushahidi tuna taarifa” -Halima Mdee
Good News kwa watumishi wote wanaoidai Serikali