Wafanyabiashara wawili ambao ni wakazi wa Kigamboni wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya kuchapisha habari katika mtando bila leseni.
Washitakiwa hao ni Obadia Kwitega na Stella Ommary ambao wamesomewa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Rwizile.
Wakili Kakula amedai kuwa washitakiwa wana kosa moja ambalo wamelitenda kati ya Januari 29 na Machi 29, 2019 katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam ambapo kupitia runinga ya mtandaoni ikijulikana kama HABARIMPYA TV walichapisha taarifa bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo, washitakiwa walikana kutenda kosa, Wakili Kakula ameeleza kuwa upelelezi haujakamilika na dhamana ipo wazi ambapo walipewa masharti yakuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Mil.5
Hata hivyo, mshitakiwa Stella ndiye aliyeweza kutimiza masharti na kuachiwa kwa dhamana, huku mwenzie akienda rumande.Kesi imeahirishwa hadi Aprili 30, 2019.