Top Stories

Ulipofikia upelelezi wa kesi ya Halima Mdee kumtolea lugha ya matusi JPM

on

Leo September 12/2017  upelelezi wa kesi ya kumtolea lugha ya matusi Rais John Magufuli inayomkabili, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee umekamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa serikali mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika nae Kishenyi amedai kuwa anaiomba mahakama hiyo, ipange tarehe kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali (PH).

Baada ya kusema hayo, wakili wa Halima Mdee, Peter Kibatala alidai kuwa wanaondoa mapingamizi yao na kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi October 11/2017 kwa ajili ya maelezo ya awali. 

Uliiona hii? KUHUSU TUNDU LISSU! ADC YALAANI, YAPAZA SAUTI

Hii je?UJANGILI! Sentensi 18 za Makamu wa Rais Mstaafu kupinga Ujangili

Soma na hizi

Tupia Comments