Kampuni inayoongoza kwa kusamabza na kupakua muziki Spotify leo imeachia orodha ya wanamuziki 10 bora kutoka Tanzania waliosikilizwa sana duniani mwaka huu wa 2021. Kupitia kampeni yao iitwayo “Wrapped 2021”, Spotify pia imeachia orodha ya nyimbo na album zilizosikilizwa zaidi kupitia mtandao huo.
Kwa mara ya kwanza, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Diamond Platnumz au ‘Simba’ ndiye msanii peke kutoka Tanzania ambaye ameingia kwenye tano bora ya wanamuziki wanaosikilizwa sana. Drake ameshika nafasi ya kwanza akifatiwa na Justin Bieber, alafu Diamond katika nafasi ya tatu. Nafasi ya nne imeshikwa na Burna Boy huku Kanye West akimalizia katika nafasi ya tano.
Kwenye orodha ya wanamuziki kutoka Tanzania wanaosikilizwa sana, Harmonize au ‘Kondeboy’ amechukua nafasi ya pili – ishara ya kwamba anaendelea kufanya vizuri kimuziki licha ya kuondoka kwenye lebo ya Wasafi. Nafasi ya tatu imeshikwa na Alikiba akifatiwa na Mbosso, kisha Rayvanny katika nafasi ya tano.
Nyimbo zilizofanya vizuri zaidi nchin Tanazaina kwa mawaka huu ni Amapiano ya Diamond – IYO (feat. Focalistic, Mapara A Jazz, & Ntosh Gazi) ikifatiwa na Loyalty (feat. Marioo & Nandy) ya Darasa, na Sukari ya Zuchu katika nafasi tatu. Hii inaonyesha kwamba Zuchu ndiye msanii wa peke wa kike ambaye nyimbo yake ime-hit kwenye kumi bora. Baikoko ya Mbosso imeshika nafasi ya nne na Ndombolo (feat. AbduKiba, K2ga & Tommy Flavour) ya Alikibameshika nafasi ya tano.
Kimataifa, Peaches ya Justin Bieber ft. Daniel Caesar & Giveon ilisikilizwa sana huku MONTERO (Call Me By Your Name) ya Lil Nas X ikichukua nafasi ya pili, na kufatiwa na Running (To You) ya Chike. Nyimbo ya The Kid LAROI iitwayo STAY ipo katika nafasi ya nne na kwa mara nyingine Lil Nas X anajitokeza katika nafasi ya tano kupitia mwimbo wake wa INDUSTRY BABY .
Ifuatayo ni orodha ya “Wrapped 2021” kutoka Spotify
Wanamuziki waliosikilzwa sana Tanzania
- Drake
- Justin Bieber
- Diamond Platnumz
- Burna Boy
- Kanye West
- Chris Brown
- Harmonize
- The Weeknd
- WizKid
- Ed Sheeran
Nyimbo zilizosikilizwa sana nchini Tanzania
- Justin Bieber – Peaches (feat. Daniel Caesar & Giveon)
- Lil Nas X – MONTERO (Call Me By Your Name)
- chike – Running (To You)
- The Kid LAROI – STAY (with Justin Bieber)
- Lil Nas X – INDUSTRY BABY (feat. Jack Harlow)
- Diamond Platnumz – IYO (feat. Focalistic, Mapara A Jazz, & Ntosh Gazi)
- Olamide – Infinity (feat. Omah Lay)
- Bruno Mars – Leave The Door Open
- JoeBoy – Sip (Alcohol)
- Dua Lipa – Levitating (feat. DaBaby)
Wanamuziki kutoka Tanzania waliosikilizwa zaidi
Nyimbo kutoka Tanzania zilizosikilizwa sana
- Diamond Platnumz – IYO (feat. Focalistic, Mapara A Jazz, & Ntosh Gazi)
- Darassa – Loyalty (feat. Marioo & Nandy)
- Zuchu – Sukari
- Mbosso – Baikoko
- Alikiba – Ndombolo (feat. AbduKiba, K2ga & Tommy Flavour)
- Marioo – For You
- Diamond Platnumz – Jeje
- Diamond Platnumz – Waah! (feat. Koffi Olomide)
- Rayvanny – Number One (feat. Zuchu)
- Marioo – Mama Amina