Mara kwa mara nimekuwa nikikusogezea orodha ya waigizaji bora duniani au msanii mwenye hela ndefu zaidi duniani au hata wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani… na najua kote huko ulikaa karibu na mimi kwenye ufuatiliaji wa hesabu hizo zote mtu wangu.
Time hii nataka niisogeze kwako orodha tofauti kabisa… Je unawajua DJ’s wenye hela zaidi duniani?! Yes DJ’s mtu wangu, na kwa mwaka 2015 jarida la Forbes la Marekani limetoa orodha ya ‘Electronic Kings 2015’ hapa utaweza kuwajua wale DJ’s wote wakubwa na wenye pesa duniani.
Kwenye Orodha hiyo yupo Calvin Harris kutoka Uingereza ambae ndiye Dj anaelipwa zaidi kwa mwaka huu akiwa na thamani ya $66 Million, anafuatiwa na David Guetta kutoka Ufaransa akiwa na thamani ya $37Million.
Wengine pia wapo, ungependa kuwajua? Orodha kamili nimeisogeza kwako hapa chini mtu wangu.
Hii hapa ni orodha ya ‘Electronic Kings 2015’…
1. Calvin Harris kutoka Uingereza – $66 Million.
2. David Guetta kutoka Ufaransa– $37 Million.
3. Tiesto kutoka Netherlands Uingereza– $36 Million
4. Skrillex kutoka Los Angeles Marekani – $24 Million.
5. Steve Aoki kutoka Miami – $24 Million.
6. Avicii kutoka Sweeden– $19 Million.
7. Zedd kutoka Urusi – $ 17 Million
8. Kevin Garrix – $ 17 Million.
9. Afrojack kutoka Netherlands Uingereza – $16 Million
10. Diplo kutoka Marekani – $15 Million.
11. Deadmau5 kutoka Canada – $15 Million.
Dj Deadmau5 hua haonyeshi sura yake na kwenye shows zake nyingi hupendelea kuvaa kichwa cha mdoli (Mickey Mouse) na ameshawahi kupiga muziki kwenye show za BET Awards zaidi ya mara 3.
Nimekusogezea na video ya Forbes pia hapa chini ikielezea kwanini hawa ndio DJ’s wanaolipwa zaidi.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos