Kwenye sehemu ya kwanza jana Mwimbaji wa Bongofleva Ommy Dimpoz aliongea na millardayo.com na AyoTV hapa Johannesburg South Africa na kukiri ni kweli chanzo cha kufanyiwa Oparesheni ni baada ya Madaktari kugundua kuwa alikunywa au kula kitu kilichowekwa sumu.
Kwenye sehemu ya pili leo, Ommy amefunguka zaidi, miongoni mwa maswali aliyoulizwa na Mtangazaji/Blogger Millard Ayo ni Aliwekewa lini sumu? Anahisi nani anahusika? Anadhani anao maadui wa kudiriki kufika mbali kiasi hicho? umakini wake kwenye kula anapojichanganya na watu ukoje?
Dimpoz pia ameonyesha sehemu ya mwili wake iliyochanwa kwa Oparesheni na kuzungumzia pia Wasanii wanaoandamwa kisa hawajampost kumpa pole, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA
EXCLUSIVE: “SUMU NDIO CHANZO CHA MIMI KUUMWA” – OMMY DIMPOZ, MTAZAME MWENYEWE AKIONGEA KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI
VIDEO: OMMY DIMPOZ ALIVYORUSHWA KICHURA NA WANAJESHI LUGALO PAMOJA NA KWAMBA WALIGUNDUA NI MSANII….. BONYEZA PLAY HAPA CHINI