Baada ya Rais Magufuli kutoa ahadi yake kwamba kabla ya kipindi chake kuisha serikali itahamia Dodoma, Dodoma imekuwa kwenye headline mbalimbali.
Ripota wa millardayo.com na Ayo TV ametembelea mji wa Dodoma na kukutana na dalali wa muda mrefu, Michael Lucas ambapo ameainisha mambo mbalimbali kuhusiana na upatikanaji wa viwanja, gharama za nyumba za kupangisha na maeneo yake yalivyo…..
- Maeneo ya watu wa hali ya chini viwanja vilikuwa milioni 2 lakini kwa sasa kiwanja hicho kwa kinauzwa milioni tano hadi sita.
- Maeneo ambayo watu wenye kipato cha juu wanaishi ni Area D, Area C na Uzunguni
- Maeneo ya kishua viwanja vilikuwa milioni 40 hadi 60 lakini kwa sasa ni milioni 150 hadi 200
- Watu wanokuja kupanga sasa hivi ni watu ambao wako serikalini wamehamishwa kutoka Dar es salaam
- Mitaa ya kawaida chumba kupangisha kwa sasa ni 70,000 hadi 80,000, sehemu za kishua ni 120,00 hadi 150,000 zamani sehemu za kishua chumba ilikuwa 60,000 hadi 70000.
- Uswahilini zamani kabla ya tamko la Rais chumba ilikuwa 20,000 kwa miezi mitatu, sasa hivi 40,000 hadi 50,000 na mkataba miezi sita.
- Mitaa ya uswahili Dodoma ni Chang’ombe au jina maarufu Gwasa
- Fremu za maduka zinapangishwa kutokana na ukubwa wa fremu, fremu ya kawaida 200,000, 500,000 ni kubwa ambayo wanakuambia ni two in one.
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV AUGUST 19 2016? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI