Ephraim Kibonde, Mussa Hussein, na wakali wengine wanaoisimamisha show ya Jahazi ya Clouds FM, leo kwenye ‘Mastori ya Town’ walikuwa wakipiga mastori na Diamond Platnumz ambaye kaachia nyimbo mpya ya ‘Nitampata Wapi’ siku chache zilizopita, na tayari imeonyesha dalili njema za kufanya vizuri baada ya kuanza kupigwa na vituo vingi vya Redio na hata TV za kubwa Afrika kama MTV.
Sehemu ya mahojiano ya Diamond kwenye Jahazi iko hapa:-
Kibonde :- “.. Wanamuziki kila mmoja huwa anakaa upande wake, wewe umekaa kwenye mapenzi zaidi.. Kwanini kwenye mapenzi zaidi?…”
Diamond :- “… Ukizungumzia mapenzi ni rahisi sana kuuza.. Hata ukiwa unazungumzia suala la pesa lakini ukiingiza kwenye mapenzi tu basi zitauzika kirahisi.. ndio maana nyimbo nyingi nikiimba nakuwa zinabase kwenye mapenzi sana…”
Kibonde : “…Nyimbo zako zimekwenda vizuri na umekwenda vizuri wakati wote, kuna nyimbo nyingine ninayoipenda hii ya ‘Mdogomdogo’ ..Nini kilikufanya ukatoka kule kwa mara nyingine tena kwa maana yake hapa ulihama hata kwenye zile style zako za kubembeleza…”
Diamond: “… Nilikuwa nimetoka kufanya Afropop halafu ilifanya vizuri sana, nikasema nikifanya tena Afropop haitaleta ladha nzuri.. Nikaona mbona Wanigeria wanafanya vya kwao sana, nikasema ngoja na mimi nichukue muziki wa kwetu pia niujaribu kuumodify halafu nitietie njonjo ninazozijua mwenyewe za kisasa hivi halafu ndo niutoe…
Kikubwa ambacho kiukweli kilinipa moyo ni kwamba kulikuwa kuna tuzo zinafanyika Marekani, imeingia kama nyimbo bora ya Kiafrika, ilikuwepo pia nyimbo ya Davido, ‘Aye’ ilikuwepo nyimbo ya Bracket inaitwa ‘Mama Africa’ na nyimbo zingine pia lakini katika nyimbo ambazo zilikuwepo ikaenda kushinda hii kama nyimbo bora ya Kiafrika… Nikaona kumbe ukifanya hivi inawezekana…”
Kusikiliza Mastori ya Town ya kwenye Jahazi la Leo, bonyeza play hapa kuisikiliza.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook