Ikiwa ni Aprili 3, 2019 tunayo story kuhusu michezo ya Upatu ambapo kwa mujibu wa sheria inaelezwa kuwa ni kinyume na sheria na adhabu yake inaweza kuwa ni miaka mitano jela ama faini ya Sh.Mil tano.
Ayo Tv na millardayo.com imezungumza na Wakili wa Kujitegemea, Leornad Manyama ambapo amesema adhabu hiyo inaweza kwenda sambamba na pia mahakama inaweza kuamuru kutaifisha mali zilizotumika katika mchezo huo.